Himid Mao kuhusu majaribio aliyofanya Ulaya na mkataba wake na Azam
Kiungo wa ulinzi wa Azam FC na timu ya taifa Himid Mao amesema alifanya majaribio aliyokwenda kufanya Denmark kwenye klabu ya Randers yalikwenda vizuri na anachosubiri sasa ni pande mbili za vilabu kufikia makubaliano ili kufanya maamuzi.
“Nilikuwa nafanya mazoezi na timu na nilifanikiwa kucheza mechi pia, wameshaniona kilichobaki ni wao kumalizana na uongozi wa Azam ili niweze kujiunga nao.”
“Mawasiliano na majadiliano bado ya yanaendelea wakala wangu ananipa ripoti kwa kila hatua inayopigwa watanzania wawe na subira chochote kinaweza kutokea.”
“Walikuwa wananifuatilia kwa muda mrefu haikuwa kama bahati, sports director wao alikuwa ananifuatilia kuanzia kwenye mechi za Azam na timu ya taifa kwa hiyo ni watu ambao wananifahamu vizuri.”
“Mkataba wangu na Azam unamalizika mwezi Novermber mwaka huu, bado tunaendelea na mazungumzo lakini kuna ofa zipo kutoka vilabu mbalimbali, naangalia ofa za nje halafu nitalinganisha na Azam halafu nitachagua niende wapi.”
Himid amekuwa katika kiwango cha juu katika misimu ya hivi karibuni kitu kinachovivutia vilabu vingi vya ndani na vya nje ya nchi kutaka kumsajili nyota huyo aliyejenga jina lake akiwa na Azam.
Post a Comment