Header Ads

BAADA YA KUIBOMOA MSN, PSG WAMEKAMILISHA CMN


PSG ilimsajili Neymar kutoka FC Barcelona na kuvunja ile safu maarufu ya ushambulizi ya MSN, yaani Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar.

Baadaye ikamnasa Kylian Mbappe kutoka AS Monaco ya Ufaransa pia ili kuweka safu ya uhakika ya ushambulizi.


Sasa uhakika, safu hiyo ambayo unaweza kuiita CMN, yaani Cavani, Mbappe na Neymar imekamilika na katika mechi dhidi ya Metz, kila mmoja amefunga wakati PSG ikishinda kwa mabao 5-1.

No comments